Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISMI, Dkt. Dorothy Gwajima, akiwa katika ziara ya kikazi kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa, amesema Serikali itapeleka vifaa kwenye majengo ya Hospitali ambazo zimekamilisha ujenzi na sio zile ambazo bado. Akawataka ambao bado wafanye bidii ili waweze kumaliza na waache malumbano na kuvutana vutana.