USIKARIBIE MAENEO HAYA ! Ni HATARI ZAIDI DUNIANI !!!

maeneo Hatari zaidi Duniani !!

Wengi wetu tunaishi katika miji na nchi salama, zilizolindwa kutokana na hatari ya aina yoyote, na wengi wetu hatuna hofu sana linapokuja swala la maeneo tunamoishi.
Hata hivyo, kuna sehemu kadhaa ambazo ni hatari kiasi cha kwamba hautatamani hata kidogo kuzizuru . Kutoka mahali ambapo tani za mamba hukusanyika kwenye karamu, hadi mahali pa hatari ambapo mtu hawezi kudhubutu kutembelea, nakusafirisha moja kwa moja hadi maeneo 10 Hatari zaidi Duniani.

10. Jangwa la Daniakil,nchini Eritrea – Karibu mahali ambapo watu wengi wanapopaita ulimwengu wa kigeni ambao pia ni mahali penye joto zaidi kwenye sayari. Kwa kupima wastani wa joto wa mwaka mzima ,sehemu hii inajoto la digrii ya sensa 34.4. sehemu hii ina joto sana kiwango cha kuwa hewa kavu na vumbi hutonya au kuunyonya unyevu kutoka kwa kinywa na macho yako .

9. Bonde la, Kamchatka, Urusi – Kulingana na hadithi, mahali hapa paligunduliwa na wawindaji wawili mnamo mwaka wa 1930 .bonde hili liko chini ya mlima wa volkano katika Jimbo la Kamchatka Mashariki mwa urusi.
Bonde hili lilipewa jina lake kutokana na mizoga ya wanyama wanaotapakaa kwenye bonde kila majira ya machipuko au spring.sehemu hii ina gesi za sumu zinazovuja kutoka ardhini.

8. Hifadhi ya Kitaifa ya Madidi, Bolivia – Mahali hapa panaweza kuwa mahali pa anuwai ya kibiolojia kote duniani. Inayo aina 1088 ya ndege na wanyama 1868 wenye uti wa mgongo . Wanyama katika mbuga hili ni kama Tapir mwenye paundi 660 na popo mdogo anayekula wadudu mwenye uzani wa gramu nne tu.

7. Volkeno ya sinabung, Indonesia – kama tunavyofahamu, Volkeno ni hatari kwa asili yake. Kwa hivyo sihitaji kukusimulia maelezo ya ni kwanini haufai kuzuru maeneo haya , lau tu kama ungependa kuchomwa kama mshikaki . Walakini, Volcano hii ya zamani ya Indonesia ililipuka hivi karibuni Februari 18, 2018 na mlipuko huo ulidumu kwa karibu dakika 5.

6. afar depression , Ethiopia – mazingira haya nchini Ethiopia ni mazingira tasa na ni eneo la vipande vitatu tofauti vya ukoko wa Dunia. Linaitwa afar triple junction kuashiria Mikutano mitatu ambapo koko hizi za dunia zinajivuta .kila upande kutoka kwa mwingine , jambo ambalo huleta kila aina ya matukio ya asili kama volkeno, nyufa, mipasuko ya dunia, kuvuja kwa gesi hatari, na chemchemi za moto.

5. Bermuda Triangle – Pia inaitwa Devils Triangle,au pembe tatu za shetani . sehemu hii ipo katika Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini na ni eneo la pembetatu kutoka mwisho wa Florida, Kisiwa cha Bermuda, na Puerto Rico.
Sehemu hii ipo katika maeneo yenye usiri Fulani wa kutisha ambao huizunguka kwa sababu ya kupotea kwa watu , au vifaa vya kuruka ambako ni kwa kushangaza. Hadithi nyingine ni pamoja na kikundi cha watupaji mabomu watano wa Torpedo ya marekani waliotoweka katika pembetatu mnamo 1945

4. kivukio cha cahill, Australia – Mamba wamekuwepo kwa mamilioni, mamilioni, na mamilioni ya miaka. Inasemkeana kuwa Walikuwa hata wakati wa dinosa na waliwala kama chakula . Mahali pa hatari zaidi kuwepo kwenye sayari linapokuja suala la mamba ni kivukio cha cahills .pana mamba wengi sana ambao hutishia maisha ya binadamu wanaovuka haswa maji yakiwa mengi.

3. Ziwa Maracaibo, Venezuela – Kuna sehemu nyingi za kupendeza Duniani . kila sehemu ina uzuri, maajabu na hatari yake . Ikiwa unatafuta mahali palipo na umeme au kama waingereza waitavyo, lightning nyingi zaidi Duniani, basi usiangalie mbali zaidi ya Ziwa la Maracaibo huko Venezuela.

2. Sumatra – Indonesia – Kuna karibu volkano 400 huko Indonesia na safu ya volkeno hizi hupitia Sumatra. Kati ya volcano hizi, vokeno 127 zinaweza lipuka wakati wowote . Licha ya Mlima Sinabung kuwa hapa, watalii lazima wajihadhari na wanyama kwa jina Orangutan, pamoja na wanyama wengine wa porini hatari.

1 San Pedro Sula – Honduras – Unaweza kufikiria kwamba maeneo hatari zaidi ulimwenguni yana uhusiano wowote na viumbe hatari wanaoishi humo, au hatari za asili. Lakini kama tujuavyo, hakuna kitu ambacho ni hatari zaidi kuliko mwanadamu. San Pedro Sula ni moja wapo ya maeneo hatari duniani na sio kwa sababu ya volkeno au mamba anayekula mwanadamu. sehemu hii ni hatari Zaidi kwa Vurugu zinazohusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya,mauaji na idadi ya magenge ya watu kama vile kundi la MS-13 na genge la 18th street gang

PRESENTER ALI: Channel maalumu ya Burudani na EXCLUSIVE interview kutoka kwa mastaa Hakikisha unaSubscribe .
SHUKRAN Ni follow kwenye mitandao ya kijamii.

INSTAGRAM : http://www.instagram.com/presenterali

TWITTER : http://www.twitter.com/presenterali

FACEBOOK:http://www.facebook.com/presenterali1

KWA MATANGAZO

PIGA : +254704589139
BARUA PEPE : alipresenter@gmail.com